Vyama vitatu vya upinzani nchini Nigeria, vimetaka uchaguzi mkuu ufutwena kurudiwa upya, kwa madai ya kuwepo kasoro nyingi na utendaji mbovu wa Tume inayosimamia uchaguzi nchini humo, INEC.

Vyama hivyo vya Peoples Democratic Party (PDP), Labour na African Democratic Congress (ADC) vimetoa tamko hilo katika mkutano wao na vyombo vya Habari katika mji mkuu wa Abuja.

Mwenyekiti wa Chama cha Labour, Julius Abure akiongea katika mkutano na wanahabari. Picha ya WN.

Viongozi wa vyama hivyo, pia waliikosoa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi – INEC na jinsi inavyoshughulikia mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura, madai yanayokuja wakati tayari mgombea wa chama Tawala Tinubu akiwa anaongoza katika majimbo 14 yaliyotangazwa kati ya 36 yaliyopo.

Mwenyekiti wa Chama cha Labour, Julius Abure amesema, “nina ishahidi juu ya udanganyifu huu wa uchaguzi, ufutwe kabisa na tunatoa wito kwa INEC kufanya uchaguzi mpya ndani ya kipindi cha dirisha kilichotolewa na sheria ya uchaguzi.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 1, 2023
Watakaoficha chakula kushakiwa kwa uhujumu uchumi