Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema wafanyabiashara ambao watakaohodhi vyakula watashitakiwa kwa kosa la Uhujumu wa Uchumi.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Februari 28, 2023 katika Mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Amesema, kwa sasa hali ya chakula ni nzuri na hivyo Serikali itachukua hatua kuhakikisha inawapa unafuu Wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika hatua nyingine, Rais Mwinyi pia amewapongeza wananchi kwa kushiriki mikutano ya hadhara bila ya uvunjifu wa amani na kuwahimiza wazungumzaji wa mikutano hiyo kuhubiri amani, utulivu na mshikamano.

Uchaguzi Nigeria: Wapinzani wataka ufutwe, Tinubu aongoza
Uchaguzi Nigeria: Waangalizi EU wakosoa utendaji wa INEC