Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameitaka Menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano, kufanya kazi kwa juhudi na upendo ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu na kuleta ufanisi.

Dkt. Yonazi ameyasema hayo hii leo Februari 28, 2023 wqkati alipowasili na kuongea na Watumishi hao, huku akiwasihi kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kuhakikishq Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea na jukumu lake la kuratibu shughuli za Serikali kiufasaha.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.

Amesema, “ikumbukwe kuwa tuna jukumu kubwa la kuwatumikia wananchi hivyo tufanye kazi kwa juhudi huku tukidumisha ushirikiano, tuendelee kudumisha upendo, weledi na kuwatumikia wananchi kiufasaha,” amesisitiza Dkt. Yonazi.

Dkt. Mwinyi asifu amani mikutano ya hadhara, akemea upotoshaji
Prof. Nombo ataka kasi kuinua sekta ya elimu