Waziri wa maji, Jumaa Aweso amewataka watendaji kutozoea shida za Wananchi na kuhimiza uwajibikaji utakaoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Waziri Aweso, ameyasema hayo katika kiko cha dharura cha Menejimenti ya Wizara pamoja na kuwaungamisha moja kwa moja kwa njia ya mtandao watendaji wote wa Sekta ya Maji mikoani.

Amesisitiza Wizara kujipanga upya na kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kushughulikia changamoto za wananchi ya dhana ya kupata huduma ya Maji.

Amesema, Wizara ya Maji inakamia kutekeleza ilani ya Chama Tawala ya upatikanaji wa huduma ya maji ya asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini ifikapo 2025.

“Serikali yetu inadhamira ya dhati ya kuwaondolea wananchi changamoto ya maji, hivyo kila mtendaji katika sekta ya maji awajibike vyema katika kusimamia jambo hili lenye maslai mapana ya nchi yetu. Tuache mazoea kwa shida za wananchi ambao tumepata dhamana ya kuwahudumia,” amesisitiza Waziri Aweso.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amewakumbusha watumishi kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa katika kutoa huduma na kuongeza mahusiano baina ya watendaji na wananchi ili kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali.

Katika kiko hicho, Aweso pia amewakaribisha watendaji walioteuliwa na Rais hivi karibuni ambao ni Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Mashabiki Real Madrid wamuwashia moto Alaba
Messi awashukuru waliompiga kura