Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria- INEC, imemtangaza mgombea wa Kiongozi wa chama cha Labour, Peter Obi kishinda uchaguzi wa Urais katika jimbo la kibiashara la Lagos  ambao ni jiji kubwa Afrika,

Obi, amepata kura 582,454, akifuatiwa na aliyekuwa Gavana wa Lagos, Bola Tinubu wa chama cha All Progressive Congress ambaye amekuwa na namba kubwa ya wafuasi, katika jimbo la Lagos kwa miaka mingi.

Mgombea wa chama cha Labour, Peter Obi. Picha ya NFS.

Kiongozi wa upinzani Atiku Abubakr, wa chama cha Peoples Democratic Party, amepata kura 75,750.

Wakati wa Kampeni, Obi alikuwa ikiwahimiza wapiga kura kuwakataa washindani wake kutoka vyama ambavyo vimeiongoza Nigeria kwa robo karne, na ambao uongozi wao umejaa ufisadi na ukosefu wa usalama.

Majeruhi wa Mwendokasi atolewa ICU
CHADEMA waitaka CCM kukamilisha miradi iliyokwama