Viongozi wa Chama cha Labour nchini Nigeria wana wasiwasi jinsi maafisa wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi – INEC wanavyosimamia uchaguzi wa urais na huenda mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Abuja, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Julius Abure alisema matokeo ya uchaguzi katika majimbo ya Lagos, Rivers, Edo na Imo yalitengenezwa.

Mwenyekiti wa chama cha Laour Taifa, Julius Abure. Picha ya PM News Nigeria.

Kufuatia hali hiyo, Abure ametoa wito kwa tume hiyo ya uchaguzi kufuta matokeo ya urais ambayo walisema yalikuwa tofauti na yale yaliyorekodiwa katika vituo vya kupigia kura.

Aidha, chama hicho cha Labor pia kimemuomba Rais Muhammadu Buhari atimize majukumu yake ya kuhakikisha uchaguzi huu wa 2023 unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.

Robertinho afichua kilichoiadhibu Vipers SC
Ajali ya Boti yauwa 58 kikiwemo kichanga