Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Mkoa wa Kagera kimeitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM kukamilisha miradi iliyokwama ikiwemo ujenzi wa stendi, miradi ya huduma za maji na kurekebisha utaratibu wa utoaji wa huduma za afya.

CHADEMA, imeyasema hayo kupitia Meya mstaafu na aliyekuwa mgombea ubunge wake wa mwaka 2020, Chief Karumuna wakati wa uzinduzi wa mikutano ya hadhara Mkoani humo.

Amesema, Serikali ya CCM inatakiwa ikamilishe miradi hiyo waliyoianzisha ili iwanufaishe wakazi wa mkoa huo kwani uwepo wake pia utasaidia kuwa chachu ya maendeleo kwa Taifa kiujumla.

Hata hivyo, hivi karibuni katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera ilikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kukamilishwa kwenye Wilaya zote za Mkoa huo.

Uchaguzi Nigeria: Peter Obi ashinda Lagos
Wadau wataka sheria viungo vya Binadamu