Majeruhi pekee wa ajali ya Basi liendalo haraka (Mwendokasi) aliyekuwa amesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili-MOI, ametondolewa chumba cha Uangalizi Maalum – ICU na baada ya afya yake kuzidi kuimarika.

Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano MOI, Patrick Mvungi amesema majeruhi pia huyo ameanza kuongea na kujitambulisha kwa jina moja la Osam, mkazi wa Manzese, jijini Dar es Salaam.

Mtembea kwa miguu huyo kabla ya ajali.

Mvungi amesema,  “Tunaomba Ndugu, jamaa au marafiki wanaomfahamu wajitokeze ili kushirikiana nasi kumuhudumia na kumfariji baada ya tukio hili kutokea na sasa anaendelea vizuri.”

Februari 22, 2023 basi la mendokasi mali ya UDART lilipata ajali wakati likijaribu kulikwepa Gari dogo na kusababisha majeruhi 37 wengi wao wakiwa ni Wanafunzi.

Uongozi ni kuwatumikia Wananchi: Dkt. Mwinyi
Uchaguzi Nigeria: Peter Obi ashinda Lagos