Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kazi kubwa ya uongozi ni kuhakikisha nchi ina amani, ili jukumu la kuwatumikia wananchi liwe rahisi.

Dkt. Mwinyi amyasema hayo hii leo Februari 27, 2023 Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana wa Viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Tanzania, wakioongozwa na kiongozi wao, Sheikh Hemed Jalala.

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi katika picha ya pamoja na ugeni wake.

Amesema, kwa muktadha huo ni wazi kuwa nchi iko pamoja, licha ya uwepo wa vyama vingi vya siasa ambavyo vintofautiana kiitikadi.

Kwa upande, Sheikh Jalala amesema wamekuwa wakimuombea dua Dkt. Mwinyi na kumpongeza kwa uongozi wake uliojaa hekima na busara huku wakifuatilia kazi ya maendeleo inayofanywa chini ya uongozi wake.

Meli ya Urusi yatia nanga Bandari ya Tanga
Majeruhi wa Mwendokasi atolewa ICU