Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA), imewafungia mita za maji wateja 6,752 za malipo kabla (prepaid Water Meters), na kuwa mamlaka inayoongoza kwa kufunga mita za maji za malipo kabla kutokana na ukuaji wa Teknolojia ya TEHAMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, Mhandisi David Pallangyo, ameyasema hayo hii leo Februari 27, 2023 wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo mbele ya waandishi wa habari, jijini Dodoma.

Amesema, kufungwa kwa mita hizo imesaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi na pia imesaidia kuondoa urundikaji wa madeni ya maji na kuongeza kuwa, “tunajivunia kuwa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira ya kwanza nchini kuwafungia wanachi wetu pamoja na taasisi mita za malipo kabla.”

Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, Mhandisi David Pallangyo

Aidha, Pallangyo amebainisha kuwa kupitia mfumo huo wa Malipo Kabla IRUWASA imefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa kwa upande wa Iringa mjini kutoka wastani wa asilimia 24.6 mwaka 2020 hadi asilimia 22.52 kwa mwezi Desemba 2022.

Ameongeza kuwa idadi ya wateja waliounganishiwa huduma ya majisafi imeongezeka kutoka 28,133 mwaka 2020 hadi 40,549 kwa mwezi Disemba 2022 na kusema kwasasa changamoto iliyopo ni uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji ,kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo hivyo.

“uchafunzi na uharibifu wa vyanzo vya maji imekuwa ni tatizo kubwa licha ya elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii ila bado tatizo hili lipo,” amesisitiza Mhandisi Pallangyo

Hata hivyo, ameitaja changamoto nyingine kuwa ni uwepo wa mtandao wa maji taka usiokidhi mahitaji ambapo mfumo uliopo wa kukusanyia na kusafirishia majitaka umewafikia wakazi wa Iringa Mjini kwa asilimia 6.8 wakati katika miji ya Kilolo na Ilula mfumo huo haupo kabisa.

Botswana, Namibia waondosha starti la paspoti
Mbegu mpya ya Mchikichi yaonesha mafanikio