Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, na mwenzake wa Namibia, Hage Geingob wametia saini makubaliano ambayo yatawaruhusu raia wao kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili bila hitaji la hati za kusafiria (paspoti).

Viongozi hao walizindua mpango wa kusafiri bila paspoti katika kivuko cha mpaka cha Mamuno.

Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, Rais wa Namibia, Hage Geingob

Hata hivyo, Rais Masisi alisema kuanzishwa kwa matumizi ya hati za utambulisho kwa usafiri ni muhimu ili kukuza umoja kati ya nchi hizo majirani na mataifa mengine ya kusini mwa Afrika

Kuanzia sasa, raia wa nchi hizo mbili za kusini mwa Afrika watahitajika tu kutoa vitambulisho vyao katika maeneo ya kuvuka.

Wadau wataka sheria viungo vya Binadamu
IRUWASA yaongoza ufungaji mita za maji malipo kabla