Klabu ya Kagera Sugar iko mbioni kuachana na kiungo wake, Abdulaziz Makame ‘Bui’ ikiwa ni miezi sita tangu aanze kukitumikia kikosi hicho akitokea Namungo aliyoachana nayo Julai mwaka jana.

Taarifa hizo zimethibitisha na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Ally Masoud ambapo amesema suala hilo lipo na wanatarajia kulikamilisha siku za karibuni baada ya mchezaji huyo kushindwa kujumuika na wenzake tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Ally Masoud amesema tayari Makame amesitishiwa mshahara wa kila mwezi kutokana na kutohudhuria kambini tangu alipoondoka mwaka jana na kwenda kwao Zanzibar.

“Kwa sasa siwezi kueleza sana juu ya hilo kwa sababu tumeelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu wa leo (jana) na KMC hivyo tutaongea baadae.”

Kwa upande wa Makame amesema ni kweli amepata barua ya kuhitajika kuhudhuria kwenye kituo chake cha kazi ingawa ataenda pindi tu atakapopata ahueni kwani bado anauguza majeraha yake ya goti.

Hata hivyo inaeleza kuwa Makame yupo kwenye mazungumzo ya kuachana na timu hiyo kwa kile kinachoelezwa kutofautiana na baadhi ya vigogo wa Benchi la Ufundi.

Sidibe wa Real Bamako amtaja Fiston Mayele
Kibu Denis kamili kuivaa Mtibwa Sugar