Kiungo mahiri wa AS Bamako ya Mali, Ibrahim Sidibe amemtaja Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Mayele, kuwa sababu ya kikosi chao kushindwa kufurukuta kwenye mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi C, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

AS Real Bamako ilikubali kichapo cha 2-0 mbele ya Young Africans juzi Jumatano (Machi 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufifisha matumaini ya timu hiyo ya mjini Bamako-Mali kufuzu Hatua ya Robo Fainali.

Sidibe amesema kitendo cha wao kuruhusu bao la mapema la Mayele dakika ya nane ya mchezo kilichangia kuwatoa mchezoni licha ya kucheza vizuri.

“Lengo letu lilikuwa ni kulinda kwanza huku tukishambulia kwa tahadhari kwani tuliamini hii ni silaha kubwa kwetu kwa sababu tunacheza ugenini ingawa jitihada zake binafsi zilifanikiwa.”

“Kiujumla tulicheza vizuri isipokuwa makosa binafsi na matumizi mazuri ya nafasi kwa wapinzani wetu yaliweza kutugharimu hivyo kutuweka kwenye mazingira mabaya ya kufuzu hatua inayofuata.” amesema Sidibe

AS Real Bamako imeendelea kubaki mkiani mwa Kundi D ikiwa na alama zake 02, huku Young Africans ikiwa ya pili na alama 07, wakati US Monastir ya Tunisia ikiwa timu ya kwanza kufuzu kutoka kwenye Kundi hilo baada ya kufikisha alama 10.

TP Mazembe ya DR Congo ambayo ilichapwa na US Monastir kwa bao 1-0 inashika nafasi ya tatu.

Tanzania yafungua ofisi za ubalozi nchini Namibia
Mzanzibari hali tete, kusepa Kagera Sugar