Taifa la China limeweka rekodi mpya Duniani kwa kuunda meli kubwa yenye uwezo wa kubeba makontena 24,116 na mizigo ya tani zaidi ya 240,000 inayotengenezwa jijini Shanghai.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Gazeti la Umma la nchini humo hii leo Machi 10, 2023 imeeleza kuwa kukamilika kwa meli hiyo, ni rekodi mpya inayoipiku Meli iliyoundwa mwaka 2022 ikiwa na uwezo wa kubeba Makontena 24,000.

Mfano wa Meli hiyo inayotarajia kubeba Makontena 24,000.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, “hii ni meli kubwa zaidi iliyoundwa na kukamilika duniani, ambayo imevunja rekodi ya “Meli ya Changyi” iliyokamilika Mwezi Juni, Mwaka 2022 yenye uwezo wa kubeba makontena 24,000.”

Hata hjivyo, Kampuni tanzu ya Shirika la Meli la China imesema tayari kazi ya uundaji huo imekamilika kwenye kituo cha matengenezo cha Changxing.

Bukoba wapitisha Bilioni 103 utekelezaji wa Maendeleo
Tafiti: Watanzania 8,500 wanahitaji huduma upandikizaji figo