Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera , limepitisha zaidi ya Shilingi 103 bilioni, katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, kwa ajili ya matumizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo .

Akizungumza katika kikao hicho hii leo Machi 10, 2023, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Gibson Godson amesema kuwa kupitia bajeti hiyo wanakwenda kutekeleza miradi iliyoshindikana kwa miaka mingi, ukiwemo wa kituo kikuu cha mabasi na soko kuu la Bukoba.

Meya wa manispaa ya Bukoba Gibson Godson akitoa ufafanuzi na kuwasilisha mapendekezo ya bajeti Mwaka wa fedha 2023/24 kwenye kikao cha madiwani.

Amesema, “baraza la madiwani manispaa ya Bukoba limeidhinisha na kupendekeza mpango wa bajeti ya Halmashauri ya manispaa ya Bukoba, kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya maendeleo yenye jumla ya shilingi bilioni 103 ikiwa ni mapendekezo yaliyo ndani ya ukomo wa bajeti ya bilioni 35 na yaliyo nje ya bajeti ni bilioni 68.”

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Bukoba, Ahmed Njovu amesema bajeti hiyo itasaidia kuendeleza miradi iliyosimama kama kituo cha magari na soko kwa ajili ya maslahi ya maendeleo kwenye halmashauri hiyo.

Baadhi ya madiwani kutoka kata za Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakisikiliza uwasilishaji wa pendekezo la bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/2024.

“Bajeti hii tutaitekeleza na tutaitetea kwasababu ya maslahi mapana ya maendeleo yetu na lengo kubwa kuhakikisha kwamba tunafanya mabadiliko katika maeneo hayo,” amesema Njovu.

Kwa upande wao, baadhi ya madiwani wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Bilele wamesema bajeti hiyo ina manufaa makubwa kwa wananchi kwani imeangalia vipaumbele vilivyowasilishwa, kutoka katika kata zao.

Hali ilivyokuwa wakati wa uwasilishaji wa pendekezo la bajeti ya Mwaka wa fedha 2023/2024.

Malalamiko mikataba ya mafunzo Vijana 400, TASAC yatoa ufafanuzi
Rekodi mpya ujenzi wa Meli, itabeba Kontena 24,000