Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma Dkt. Alphonce Chandika amesema sheria za nchi haziruhusu kuuza viungo vya Binadamu, kauli inayokuja kufuatia kupokea simu za baadhi ya Vijana wanaohitaji kuuza figo zao.

Dkt. Chandika ameyasema hayo hilo leo Machi 13, 2023 Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma na Tokushukai Group toka Japan.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika.

Amesema, “nimepigiwa na vijana si chini ya wanne baada ya kupata namba yangu nikijua wanauliza huduma za hapa Hospitali kumbe wanataka wauze hivyo tukaona ni vema tutumie wasaa huu kuelimisha Jamii kuwa sheria za nchi haziruhusu biashara za viungo vya Binadamu.”

Aidha, Dkt. Chandika amesema kwa kipindi hicho cha miaka mitano Watanzania 33 wamefanikiwa kupandikizwa figo na 22 kati yao walipandikizwa na Madaktari wa kitanzania.

Majaliwa aifagilia GGML kuwawezesha Wanawake kielimu
Clifford Mario Ndimbo aula tena CAF