Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema hakufanikiwa alipomuomba babake amtume yeye na wanajeshi wake nchini Kenya kukabiliana na wahuni waliovamia shamba la Uhuru Kenyatta Kaskazini mwa nchi hiyo Machi 27, 2023.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Muhoozi aaliandika kuwa, “nilimwomba Mzee (Museveni) anipeleke kama kamanda mkuu katika Northlands (Shamba la Ruiru, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya), tulichohitaji ni wanajeshi 200 wa Uganda People’s Defence Force (UPDF) kuleta utulivu na nilimwambia kwamba Wakenya walihitaji kipigo kizuri, lakini mzee alikataa.”

Katika tweet nyingine, Muhoozi aliwataja Wakenya kama wezi wakubwa ambao wanahitaji kugeuzwa kuwa supu ya nyanya kufuatia uvamizi wa shamba hilo la familia ya Kenyatta, iliyopoteza Kondoo zaidi ya kondoo 1,500 na miti kadhaa ya mikaratusi ambayo ilikatwa.

Aidha, Muhoozi pia alimtaja Uhuru Kenyatta kama kaka yake mkubwa kwenye tweet nyingine ambazo zote zilichapishwa Jumamosi April Mosi, 2023, huku akisema kila kitu kinafaa kufanywa ili kumlinda rais huyo wa zamani wa Kenya, huku tweet hizo zikitafsiriwa kama kejeli kwa Wakenya.

Majaliwa awapa neno Wakuu wa mikoa, ataka utekelezaji
Mikel Arteta: Arsenal mapambano yanaendelea