Serikali ya Kenya, imetangaza majina ya Wabunge saba wa kwanza watakao shiriki katika mazungumzo naViongozi wa upinzani wakiongozwa Raila Odinga ili kumaliza uhasama wa kisiasa kati ya pande hizo mbili juu ya husu hali ngumu ya maisha, ufufuaji wa uchumi na kuundwa kwa tume ya uchaguzi IEBC na kuwepo kwa makubaliano ya kisiasa..

Hata hivyo, tangazo hilo linakuja huku Chama tawala kikisema hakitashiriki mazungumzo yoyote yatakayohusu kurejeshwa kazini kwa makamishna wanne wa IEBC, waliofutwa kazi na Rais Ruto pamoja na uwepo katika harakati za ufunguaji wa seva za uchaguzi.

Majadiliano hayo, si ishara ya udhaifu wala njia ya kuishinikiza serikali kukubaliana na matakwa ya wapinzani wake, na upinzani umewasilisha mapendekezo saba ya mazungumzo ikiwemo hatua za haraka za kupunguza bei za unga, umeme na mafuta na ada za shule, na kutaka ukaguzi wa kitaalamu wa seva zinazotumiwa na IEBC kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa urais 2022

Mazungumzo hayo, yanayotarajiwa kufanyika katika mfumo wa bunge na yatahudhuriwa na wabunge wa chama tawala ambao ni pamoja na Boni Khalwale, Hillary Sigei, Adan Keynan, Lydia Haika, George Murugara, Essy Okenyuri na Mwengi Mutuse.

Morice Chukwu: Tulifurahi Kupangiwa Young Africans
AC Milan kumtwaa jumla jumla Brahim Diaz