Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesisitiza kuendeleza maandamano kama ilivyopangwa, huku akizikosoa nchi za magharibi kwa kujaribu kuingilia masuala ya ndani ya ndani na kusema Wakenya wanaweza kusuluhisha mambo yao.

Kauli ya Odinga, inakuja wakati ambapo Serikali inasisitiza kutovumilia maandamano ya vurugu ambapo pia amewaonya wanadiplomasia wa kimataifa wanaojaribu kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake, akisema shida zinazoikabili nchi zitatatuliwa na wakenya wenyewe.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga. Picha ya Nation Media Group.

Hata hivyo, katika upande wa pili Naibu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amesema uchumi wa nchi utatatizika ikiwa maandamano yanayoendelea hayatakoma, na kusisitiza Serikali kutobadili msimamo.

Rais wa Kenya, William Ruto. Picha ya Global Bar Magazine.

Katika hotuba yake kwa wananchi, Gachagua amesema hawatayumbishwa na wale aliowaita wanasiasa wabinafsi wanaotaka kutumia mlango wa nyuma kuingia Serikalini na kusema “Machafuko yanayoelekezwa kwa raia wa Kenya na Raila Odinga yanajaribu kutusukuma kuingia katika mapatano suala ambalo haliwezekani.”

Wakati haya yakiendelea, Rais wa Kenya, William Ruto anendelea na ziara yake barani Ulaya akiwa ameelekea nchini Ubelgiji baada ya kutoka Ujerumani na alisisitiza kuhusu utawala wa Sheria akisema hatawavumulia wale wanaovunja sheria.

Ruvu Shooting kumaliza Ligi Kuu kibingwa
Mradi ufugaji Nyuki kuvinufaisha Vijiji Kigoma