Uongozi wa Klabu ya Ruvu Shooting umeweka wazi mpango mkubwa kwenye michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23, ni kufanya kazi kweli kweli kwa wachezaji wao, kuhakikisha wanavuja jasho ili wapate alama tatu.

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kazi kubwa ambayo ipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ilizobaki ni kucheza kwa juhudi na kupata matokeo mazuri.

“Tuna kazi ngumu kwenye michezo ambayo imebaki ni migumu lakini hatuna mashaka tutafanya kazi kweli kweli kutafuta ushindi, kwani inawezekana kutokana na wachezaji kuwa tayari.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi, sisi Ruvu Shooting tunajua kwamba wanahitaji matokeo mazuri nasi pia tunahitaji matokeo mazuri,” amesema Bwire.

Timu hiyo haina mwenendo mzuri ikiwa imekusanya alama 20 baada ya kucheza michezo 25 na ipo nafasi ya 15.

Young Africans matumaini kibao Lubumbashi
Odinga azionya nchi za Magharibi kuingilia mambo ya Kenya