Kikosi cha timu ya Kagera sugar (Wanankurukumbi), tayari kimeanza mazoezi ya maandalizi ya ligi kuu ya NBC Premier League katika uwanja wa Kaitaba uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera baada ya mapumziko ya mda mfupi ya kupisha michezo ya kimataifa.

Ikiwa mchezo wao wa kwanza utachezwa April 11 dhidi ya Yanga katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam, kocha wa kikosi hicho cha wanankurukumbi Meck Mexime amesema kuwa maandalizi yanaenda vizuri ya kukabiliana na mchezo dhidi ya Yanga na michezo mingine.

Wachezaji wa Kagera sugar wakifanya mazoezi uwanja wa Kaitaba.

“Kikubwa sisi tunajiandaa ili tuweze kupata alama tatu, tarehe 11 tunacheza na Yanga, tunajua tunacheza na timu ya aina gani, timu ambayo inaongoza ligi, timu ambayo inatetea ubingwa kwahiyo tunajua tunaenda kukutana na ugumu kiasi gani” Kocha Mexime.

Mchezo wa kwanza msimu huu uliochezwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, Kagera sugar alipoteza alama tatu kwa kufungwa na Yanga goli moja kwa sifuri.

Elimu uhifadhi Ruaha, Mwanakijiji asalimisha Silaha
Mfahamu Kamala Harris, jembe lenye damu ya kihindi... anachoijia Tanzania