Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar, umesema kuwa, michezo ambayo imebaki watafanya jitihada kupata matokeo mazuri yatakayowapa nafasi ya kubaki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2023/24.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema wanatambua ushindani ni mkubwa jambo linalowafanya wajipange kwa umakini.

“Ligi ni ngumu na tuna michezo ambayo imebaki, hiyo ni lazima tupambane kufanya vizuri ili kuwa kwenye nafasi nzuri ya kubaki ndani ya ligi, kushuka sio kitu ambacho tunafikiria.”

“Unajua kwa namna ligi ilivyo na michezo ambayo imebaki ukipoteza alama tatu lazima uangalie pale ambapo umekosea ili kuwa bora Kwa michezo inayofuata,” amesema Kifaru. Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 29 baada ya kucheza michezo 25.

Kiungo Rivers Unites atuma salamu nzito Simba SC
Kocha Yanga Princess atimuliwa