Uongozi wa Klabu ya Young Africans umetagaza kusitisha mkataba wa Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake ya klabu hiyo Yanga Princess Sebastian Nkoma, kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho katika mshike mshike wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Young Africans imethibitisha taarifa za kusitishwa kwa mkataba wa kocha huyo kupitia taarifa maalum iliyosambazwa katika vyanzo vya habari vya klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Maamuzi hayo yametoa nafasi kwa mchezaji wa zamani wa Young Africans Fredy Mbuna kuwa kocha wa muda wa Yanga Princess.

Taarifa ya kusitishwa kwa mkataba wa kocha Nkoma imeeleza: Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kuutarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake, Yanga Pirincess, Sebastian Nkoma.

Uamuzi huu umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Uongozi wa Yanga unamshukuru Kocha Sebastian kwa kazi yake kipindi

chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya Wanawake.

Kwa sasa benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka msimu huu utakapomalizika.

Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu

Young Africans Sports Club

28.03.2023

Mtibwa Sugar: Hatushuki daraja
Moses Phiri kukiwasha tena Simba SC