Kiungo kutoka nchini Nigeria na Klabu bingwa nchini humo Rivers United Joseph Onoja amesema endapo atafanikiwa kutua Simba SC mwishoni mwa msimu huu, basi yupo tayari kupambania namba mbele ya viungo Sadio Kanoute (Mali) na Mzamiru Yassin (Tanzania).

Onaja aliingia katika kikosi bora cha mzunguumo watano wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika pamoja na wachezaji watatu wa Simba Jean Baleke, Clatous Chama na Kanoute.

Kiungo huyo ni kati ya nyota wanaotajwa kuwa katika orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Simba SC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya kimataifa inayoratibiwa na CAF.

Onoja amesema kama mipango ya kujiunga na Simba SC itakamilika, basi hatakubali kukaa Benchi na badala yake ataingia katika kikosi cha kwanza kwa kumshawisho Kocha Mkuu Robertinho na wasaidizi wake.

amesema anaheshimu ubora na kiwango cha kila mchezaji ndani ya Simba SC, lakini hiyo haimfanyi aogope kupambania namba na kuingia katika kikosi cha kwanza.

“Mimi nimezaliwa kupambana, kila sehemu nilipokwenda kucheza nimekuwa nikikutana ushindani wa namba ambao unanifanya niongeze bidii ya kupambana ili niingie katika kikosi cha kwanza.”

“Simba ninaifahamu na nimekuwa nikiifutilia kwa karibu, nawafahamu wachezaji baadhi katika timu hiyo, ambayo ninaamini nikijiunga nayo basi nitaingia katika kikosi cha kwanza,” amesema Onoja.

Upo uwezekano mkubwa wa Simba SC kuachana na kiungo wake Ismail Sawadogo aliyejiunga na timu hiyo katika usajili wa Dirisha Dogo msimu huu baada ya mchezaji huyo kushindwa kuonesha upinzani mbele ya Mzamiru na Kanoute.

Ousmane Kamissoko kuongeza nguvu Young Africans
Mtibwa Sugar: Hatushuki daraja