Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtu mmoja Elias Bukumie (32), akikabiliwa na tuhuma za kumuuwa mtoto wake wa umri wa miaka mitano mwenye ulemavu wa viungo, kisha kumzika porini kwa madai ya kushindwa kuendelea kumlea.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amesema baada ya kumkamata baba wa mtoto huyo alikiri kumuua mwanaye akidai alitekeleza mauaji hayo kwani alishindwa kuendelea kumlea mwenyewe baada ya mkewe kumkimbia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo.

Amesema, “alikuwa akiishi na mkewe na mwezi uliopita mkewe alimuacha akarudi kwa wazazi wake, alipoona anashindwa kuendelea kumlea, alimpeleka kwa mkewe ambaye alikuwa kwa wazazi wake na alipofika wazazi wa mwanamke walikataa kumpokea mtoto na kumtaka arudi naye.”

Aidha, Kamanda Jongo amesema mwili wa mtoto huyo uligunduliwa huko porini na wasamaria wema na kwamba taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza kumfikisha mtuhumiwa mahakamani huku akiitaka jamii kutoa taarifa Polisi pale wanapobaini ukatili dhidi ya watoto.

32 watupwa jela umiliki silaha kinyume cha sheria
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 14, 2023