Mchungaji Paul Mackenzie ambaye ni muhubiri wa kanisa la Good news International amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya na anazuiliwa katika kituo cha Malindi, kutokana na mauaji ya watu wanne.

Watu hao, waliofariki April 13, 2023 baada ya kudaiwa kuwalazimisha waumini wake kufunga kula na kunywa kwa muda, ili kufariki na kwenda kumuona Mungu wao.

Mshukiwa huyo ambaye amekua akidaiwa kuendesha mahubiri yenye itikadi kali katike eneo la Shakahola, anatarajiwa kufikishwa mahakama siku ya Jumatatu Aprili 17, 2023.

Katika sakata hilo, watu wengine 11 wamelazwa Hospitalini kutokana na kuathiriwa na mfungo huo na hivyo kupelekea kudhohofika na hali zao inasemekana ni mbaya huku wakiendelea kupatiwa matibabu.

Jasmin Razack: Feisal ana haki ya kuvunja mkataba
Wakala afichua usajili wa Baleke Simba SC