Idara ya upelelezi DCI eneo la Malindi imeanzisha uchunguzi, baada ya kupata habari kuwa bado kuna watu zaidi katika msitu mmoja eneo la Shakahola, kijiji ambapo watu 15 walipatikana jana wakiwa mahututi wakidaiwa kufunga ili kufa, baada ya kushawishiwa na Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International.

Polisi nchini Kenya inasema watu watatu kati ya 11 waliokua wakipokea matibabu katika hospitali ya Malindi wako katika hali mbaya ya kiafya na wanaendelea kupata matibabu huku wengine nane wakiwa katika hali nzuri baada ya kutibiwa hapo jana Aprili 13, 2023.

Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International.

Hata hivyo, Polisi mjini Malindi wamesema tayari wameanza msako wa kumpata Kasisi mmoja kwa jina Paul McKenzie anyedaiwa kusababisha vifo vya waumini 4 eneo hilo, baada ya kasisi huyo wa kudaiwa kuwashawishi waumini hao kutokula wala kunywa kwa siku kadhaa.

Hata hivyo, baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, Polisi walifanikiwa kuwaokoa watu 15, sita kati yao wakiwa katika hali mahututi na kukimbizwa hospitali ya Malindi ambapi wanne walifariki.

Serikali yataka miradi ikamilike kwa ubora, wakati
Waziri Mkuu atoa wito vita mmomonyoko wa maadili