Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ambaye pia amewasihi watanzania kujenga mshikamano na kuliinua Taifa kiuchumi ili kuacha alama ambayo itakuwa ni somo kwa vizazi vijavyo.
Biteko ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe ameyasema hayo mara baada ya kushiriki Futari na baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Biteko amewataka wananchi wa Bukombe kuungana katika dini zao ili kudumisha amani na mshikamano walionao katika wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.
Amesema, “tukishikamana tutalijenda Taifa na tutakapokuwa wazee tutakuwa na la kujivunia kwa watoto wetu tukiwaonesha kwamba sisi tulifanya hili na tulijenga hiki ili kuwapa hamasa katikia ukuaji wao.”