Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ‘TPLB’ imethibitisha mchezo wa Young Africans dhidi ya Singida Big Stars utachezwa Jumanne (Mei 04) katika Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida.

Mchezo huo wa Ligi Kuu uliopangwa kuanza saa kumi jioni, ulileta utata kufuatia timu za Young Africans na Singida Big Stars kutinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na ilifahamika miamba hiyo itakutana katika Uwanja wa CCM Liti.

Taarifa ya TPLB na TFF zimethibitsiha kuwa miamba hiyo itaaanza kucheza mchezo wa Ligi Kuu Mei 04, kisha itakutana tena katika Uwanja wa CCM Liti kwa mara ya pili mfululizo Mei 07 kwenye mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Mchezo mwingine wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ utapigwa Mei 06 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC.

Kabla ya mchezo huo Simba SC itakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC itakayokuwa nyumbani katika Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi Mei 03, huku Azam FC itakuwa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, April 22.

Tusambaze ukuzaji viumbe maji nchi nzima - Dkt. Mlima
Polisi, wadau watoa mafunzo kwa Madereva wa Utalii