Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza, Dominic Raab amejiuzulu kufuatia madai ya uonevu dhidi yake, yaliyothibitishwa katika ripoti iliyokabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Rishi Sunak hatua ambayo huenda ikatikisa chama cha Conservative.

Kujiuzulu kwa Raab, ni pigo kwa waziri mkuu Rishi Sunak, ikizingatiwa kuwa ni wiki mbili zimesalia kabla ya uchaguzi wa wabunge kuandaliwa na mwaka 2020 aliwahi kusema angejiuzulu iwapo kutatokea madai yoyote dhidi yake.

Sunak pia anakabiliwa kibarua kigumu cha kuweka chama chake kuwa imara ili kisipoteze kwa upinzani, wakati huu uchaguzi mkuu ukitarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Katia barua yake ya kujiuzulu, Raab ameandika kuwa, “Ingawa ninahisi kuwa na wajibu wa kukubali matokeo ya uchunguzi huo, ilitupilia mbali madai yote isipokuwa mawili yaliyotolewa dhidi yangu, pia ninaamini kuwa matokeo yake mawili mabaya yana dosari na yanaweka mfano wa hatari kwa mwenendo wa serikali nzuri.”

Raab pia amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wa waziri wa haki, ambapo alikuwa anakabiliana na mrundiko wa kesi za uhalifu, kutokana na ufadhili mdogo na Uviko-19.

Mauricio Pochettino kurudi tena London?
Gabriel Geay afichua siri Boston Marathon 2023