Nchi za Kiafrika zinajipanga kuidhinisha chanjo mpya ya malaria, na dozi milioni 20 mwaka huu, baada ya mamlaka ya udhibiti wa dawa nchini Nigeria kuungana na Ghana katika kusaidia chanjo mpya ya R21 ambapo zitakuwa za kwanza duniani kuingia katika rekodi hiyo.
Nigeria na Ghana ambazo hazina rasilimali nyingi za udhibiti wa dawa, hapo awali zilitegemea shirika la Umoja wa Mataifa kuhakiki dawa mpya ambapo kwasasa, kuna ukosefu wa ufikiaji wa umma kwa taarifa za kina kuhusu matokeo ya chanjo ya malaria katika majaribio makubwa.
Hata hivyo, udharura wa kushughulikia ugonjwa unaoua zaidi ya watu 600,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, na juhudi za hivi karibuni za kuimarisha usimamizi wa madawa ya kulevya katika eneo hilo, zinabadilisha mchakato huo.
Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, lilisema katika mkutano wa ngazi ya juu wiki hii kwamba mamlaka za udhibiti kutoka angalau nchi 10 za Afrika kwa sasa zinachunguza data za majaribio, ili kutathmini chanjo hiyo huku ikitarajiwa kuwa nchi za ziada zitatoa idhini ya chanjo hiyo katika wiki chache zijazo.