Oparesheni ya kufukua makaburi eneo la Shakahola mjini Malindi imeingia siku yake ya nne hii leo Aprili 22, 2023 huku maafisa wa upelelezi wakisema wamefukua miili 10.

Miongoni mwa miili iliyofukuliwa hii leo katika shamba la mhubiri huyo Paul Makenzi ni familia ya watu watano, baba mama na wanawawe watatu, ambao walikua wamezikwa sehemu moja.

Maafisa hao wa idara ya upelelezi DCI, kitengo maalum cha jinai jana Aprili 21, 2023 walisema wamefanikiwa kuifukua miili ya watu watatu akiwemo mama na watoto wawili waliokutwa wamezikwa katika kaburi moja.

Watu wengine 11, walifariki April 13, 2023 kutokana Mtuhumiwa huyo Makenzie ambaye anadaiwa kuendesha mahubiri yenye itikadi kali katika eneo la Shakahola na alifikishwa mahakama siku ya Jumatatu Aprili 17, 2023 akituhumiwa kuwashawishi waumini hao kufunga na wasile wala kunywa hadi wafe ili wakakutane na MUNGU.

Serikali kushirikiana na taasisi ufanikishaji wanaoenda Hijja
Afrika yajipanga kuidhinisha chanjo mpya ya Malaria