Maafisa wa idara ya upelelezi DCI, kitengo maalum cha jinai wamefanikiwa kuifukua miili ya watu watatu waliozikwa kwenye shamba la mhubiri tata, Paul Mackenzie.

Ufukuaji huo wa makaburi umefanyika katika eneo la Shakahola lililopo Malindi, ambapo miili ya wanaoaminika kuwa ni washirika wake iliopolewa.

Miili hiyo ni ya watu watatu akiwemo mama na watoto wawili na Polisi inasema mama na mtoto mdogo wamekutwa wamezikwa katika kaburi moja.

Jana, Aprili 20, 2023 ilitolewa taarifa kuwa, mwanamke mmoja ameokolewa akiwa amedhoofika msituni kutokana na makali ya njaa na kukimbizwa katika kituo cha Afya kwa matibabu mjini Malindi, huku maafisa wa Upelelezi wa jinai wakitambua makaburi 12 ya watu wanaodaiwa kuzikwa kwenye shamba la mhubiri huyo.

Mapema Wiki iliyopita, Mchungaji huyo aliondolewa dhamana aliyopewa, ambapo Hakimu Mkuu, Elizabeth Usui alisema mtuhumiwa huyo amekuwa akiendeleza vitendo vyake eneo la Shakahola – Kilifi, licha ya kuzuiliwa kufanya hivyo na kesi yake itatajwa tena Mei 2, baada ya uchunguzi kukamilika.

Watu wengine 11, walifariki April 13, 2023 kutokana na tukio hilo na Mtuhumiwa huyo Makenzie ambaye amekua akidaiwa kuendesha mahubiri yenye itikadi kali katika eneo la Shakahola na alifikishwa mahakama siku ya Jumatatu Aprili 17, 2023 akituhumiwa kuwashawishi waumini hao kufunga na wasile wala kunywa hadi wafe ili wakakutane na MUNGU wao.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 22, 2023
Zinchenko arudi kundini Arsenal