Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, John Heche amesema hadhani kama Mwigulu Nchemba anafaa na kuitendea haki nafasi yake Waziri wa Fedha, na badala yake anaweza kushika nafasi nyingine kwani hana mipango thabiti ya kuinua uchumi wa nchi kiasi hata ngano inaagizwa kutoka nje.

Heche ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na Dar24 Media na kuongeza kuwa hali hiyo inaweza kusababisha nchi kulala njaa siku moja na ni aibu kwa Taifa kubwa lenye ardhi yenye rutuba karibu kila mkoa na hali ya ustawishaji wa mimea kuagiza chakula nje.

Amesema, ” halafu ngano yenyewe inaagizwa kutoka Ukraine na huko kuna vita inaendelea siku moja tutalala na njaa kama Taifa, me sidhani kama mwigulu anafaa kuwa Waziri wa Fedha kwa kuwa hana mipango ya kuipeleka mbele nchi kiuchumi hii ni hatari.”

Aidha, Heche ameongeza kuwa nchi imekuwa ikienda bila malengo kutokana na utashi wa baadhi ya watu kufanya maamuzi bila kujali wala kushirikisha wengine, na kwamba mfumo uliopo hauangalii ni nani anaweza kufanya nini na badala yake unawachagua watu ili kuziba nafasi na kupeana ulaji.

Masau Bwire akiri mambo magumu Ruvu Shooting
Jean Baleke aichimba mkwara Wydad AC