Kijana mmoja, Somnath Mhatre wa Mumbai nchini India amefariki dunia baada ya kutaka kupiga picha huku akimubusu nyoka aina Cobra, kwa ajili ya kuweka picha hizo katika mitandao ya kijamii.

Kijana huyo ambaye alikua akifanya kazi katika kikosi cha kudhibiti nyoka wenye sumu kali alikuwa ameagizwa na mabosi wake katika mji wa Mumbai kumkamata nyoka huyo aliyeingia ndani ya gari la raia.

Akiwa eneo la tukio, kijana huyo alifanikiwa kumkamata nyoka na kumdhibiti kisha akaanza kumchezea na kutaka kupiga naye picha huku akiwa anamubusu jambo ambalo lilisababisha nyoka huyo kumdhuru.

Mashuhuda wanasema Nyoka huyo alimuuma Somnath mdomoni na usoni na kumtemea sumu hali ambayo ilisababisha kulegea na kukimbizwa hospitali na alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake.

Viongozi wa dini tupo tayari kupimwa: Sheikh Kakulukulu
Serikali yawatua mzigo wadaiwa pango la Ardhi