Watu 10 wa familia moja wameuawa katika mji wa Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini, baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na silaha. 

Taarifa ya Waziri  anayehusika na masuala ya Polisi nchini humo, Bheki Cele imeeleza kuwa mpaka sasa bado haijafahamika sababu hasa za kutekelezwa kwa mauaji hayo, na kwamba wanaendelea kuchunguza tukio hilo la kushtukiza.

Cele ambaye alikuwa akitoa taarifa hiyo Mkoani KwaZulu-Natal, amesema waliouawa ni Wanawake saba na wanaume watatu,  na kwamba hali katika eneo hilo ni ya kusikitisha.

Mapema mwezi Januari 2023, tukio lingine kama hilo liliripotiwa, ambapo watu wenye silaha waliwauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine watatu wakati wakishiriki sherehe ya kuzaliwa (Birthday( ya mtu mmoja kati yao, mjini Gqeberha. 

Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi duniani, ambazo zina visa vingi vya mauaji vinatokana na watu kuuawa kwa risasi au kuuawa, huku takwimu zionesha kuwa takriban watu 20,000 huuawa kila mwaka.

Rais Samia amteua Jaji Masaju, Dkt. Mayungi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 22, 2023