Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa usiku imesema Maelfu ya wakimbizi wa Sudan wamekuwa wakiwasili katika nchi jirani ya Chad tangu mwishoni mwa wiki yalipoanza mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 200.

Kuwasili kwao huko kunatokana na mapigano yanayoendelea jijini Khartoum nchini Sudan, tangu Jumamosi Aprili 15, kati ya vikosi vya msaada wa haraka – RSF, vinavyoongozwa na Jenerali Mohammed Hamdane Daglo na jeshi la kitaifa linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema, “makadirio ya wakimbizi wapya ambao wamewasili Mashariki mwa Chad katika siku mbili zilizopita ni kati ya 10,000 hadi 20,000”, taarifa ambayo imeandikwa pia kupitia ukurasa wake wa Twitter wa Laura Lo Castro, ambaye mwakilishi wa UNHCR nchini Chad.

Ujumbe wa pamoja wa UNHCR, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP umesema umeshuhudia wimbi la wakimbizi wapya wa Sudan wanaokimbia mapigano nchini mwao, katika maeneo matatu ya kwanza ambayo yalitukia siku ya Jumanne Aprili 18, 2023.

Serikali yaomba muda suala la ATCL
Hofu yatanda Nigeria, VAR tishio Young Africans