Serikali ya Tanzania imesema imesikitishwa na hali ya uzorotaji wa amani na usalama nchini Sudan huku ikiungana na Baraza la Amani la Usalama la Umoja wa Afrika kulaani mapigano yanayoendelea nchini humo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax ambaye ameongeza kuwa Tanzania inatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea na pande zinazohusika katika mgogoro huo tafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo.

Amesema, “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasikitishwa na hali inayoendelea, kama mjumbe wa Baraza la Amani la Usalama la Umoja wa inaunga mkono tamko la Baraza la Aprili 16, 2023 kulaani mapigano yanayoendelea nchini Sudan.”

Aidha, Dkt. Tax ameongeza kuwa pande hizo pia zinapaswa kuhakikisha mahitaji ya raia wa Sudan na wale wa nchi nyingine yanapatikana na kwamba inafuatilia kwa ukaribu raia wake (210), waishio nchini humo ambapo 171 ni Wanafunzi na waliosalia ni Maafisa wa Ubalozi na raia wengine ili kujua maendeleo yao.

Hata hivyo amesema hadi kufikia sasa hakuna Mtanzania yeyote aliyeripotiwa kuathiriwa na mapigano hayo, na kwamba Blozi wa Tanzania nchini humo Silimba Kombo Haji anaendelea na majukumu yake kuhakikisha usalama wa Watanzani hao.

Meyele awashusha PRESHA mashabiki Young Africans
Rekodi za mwamuzi Simba SC VS Wydad AC