Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linachunguza tukio la vifo vya watu wanne wa
familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye
jenereta walilowasha ndani ya nyumba na baadae kulala, tukio ambalo limetokea Aprili 19, 2023
maeneo ya Chang’ombe, Temeke, Jijini Dar es salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa tarehe 18. 04. 2023 majira ya saa 4 :00 usiku watu hao waliwasha jenereta
baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba na uchunguzi wa awali unaonesha kuwa
watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni chafu ya moshi
iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.

Waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim (7), Munira Ibrahim (6) Muyyat
Ibrahim (3). Mume na mke ambao ni Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu (29) wote wakazi wa
Kilimahewa, Chang’ombe hali zao sio nzuri an wanenedelea kupatiwa matibabu katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa
kushirikiana na mamlaka zingine za Serikali.

Erling Haaland kufungwa pingu mpya Man City
Andrew Simchimba aota ufungaji bora ASFC