Mwandishi wa Habari na Mtangazaji Emanuel Victor Mdoe (41), wa Abood Media ya Mkoani Morogoro amefariki kwa ajali ya gari iliyotokea usikuwa kuamkia hii leo Aprili 20, 2023.

Marehemu Emanuel Victor Mdoe.

Emanuel ambaye alikuwa ni maarufu kwa jina la Ima one, alipata ajali wakati akirejea nyumbani kwake eneo la Mkambarani mjini Mrorogoro na akiwa na gari ndogo aina ya Toyota IST, yenye namba za usajili T 204 DNX .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoa Morogoro, Alex Mkama amesema ajali hiyohiyo imesababishwa na mwendokasi na ilitokea eneo la mkambarani lililopo Barabara kuu ya Morogoro – Dar es salam.

Mwili wa Mtangazaji huyo, umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya taratibu za maziko.

Singida B.S: Hatuna papara na Young Africans
Miradi ya Mazingira kutekelezwa kwa Viwango - Serikali