Takriban Watu 78 wameuawa kufuatia mkanyagano katika shule moja iliyopo mji mkuu wa Yemen Sanaa, wakati wa hafla ya kusambaza misaada kwa ajili ya ramadhani.

Tukio hilo limetokea  katika Jiji la Kale katikati mwa mji huo, wakati mamia ya watu masikini walipokusanyika katika hafla iliyoandaliwa na wafanyabiashara, ya kutoa msaada na waratibu wa mgao huo wanazuiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa msemaji wa wazara ya mambo ya ndani, tukio hilo lilisababishwa na ukosefu wa uratibu mwafaka kutoka kwa mamlaka za mitaa wakati wa kugawa nasimu za fedha ambapo majeruhi walipelekwa katika hospitali za karibu kupata huduma za matibabu.

Matukio ya fujo baada ya tukio hilo yalionekana katika picha za video katika eneo la Bab-al-Yemen mjini humo huku mamia ya watu wakisadikika kufika katika shule hiyo kupokea michango ambayo ilikuwa takriban $9 (£7) kwa kila mtu.

Wanajeshi wa Sudan waliokimbia mapigano wajisalimisha
Harry Kane awindwa Paris, Munich