Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa wito kwa Vyombo vya habari, Mitandao ya kijamii na makampuni ya simu kuhakikisha wanakuwa na mipango endelevu ya kuifanya Tanzania inakuwa na Ziro’ Malaria.
Nape ameyasema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2023 ambayo Kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake.
“Naomba nielekeze Vymobo vya Habari, hakikisheni mnakuwa na mpango endelevu wa kuhakikisha Tanzania inakuwa na Zero Malaria kila chombo, tukishikamana kwa pamoja inawezekana hii siyo kazi ya Wizara ya Afya peke yake,” amesisitiza Waziri Nape.
Aidha nape amesema Tanzania bila Malaria inawezekana na kwamba vyombo vya Habari vipo vingi na hivyo kwa kushikamana kwa pamoja kuielimisha jamii juu ya madhara ya ugonjwa huo na namna ya kuchukua tahadhari ni wazi kuwa lengio litafanikiwa.