Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amethibitisha kuongezeka kwa kifo cha mtu mmoja wa ugonjwa wa Marburg hali inayopelekea kufikia jumla ya visa vya vifo 6 mpaka sasa tangu ugonjwa huo uibuke mkoani Kagera.

Amethibitisha hayo wakati akiongea na wavuvi na wananchi wa mwalo wa Nyamkazi baada ya kukabidhi boti kwa wavuvi hao kama sehemu ya shukrani kwa ushiriki wa kuokoa abiria baada ya ajali ya precision kutokea mnamo Novemba 9 Mwaka jana.

Amesema “ninayo furaha kuwaambia kwamba waliofariki mpaka sasa wako sita, wagonjwa waliopona wapo na wale tuliokuwa tumewaweka karantini wote hakuna hata mmoja anayeumwa na wote wameshatoka”.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wizara ya afya kuudhibiti mapema ugonjwa huo.

“Tunashukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na wizara ya afya laiti wasingekuwa haraka inawezekana wangekufa zaidi ya watu 700 hapa.

Lukaku aipotezea Chelsea, ajikita Inter Milan
Pluijm aitangazia vita Young Africans