Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko – CPB, Salum Awadh ametangaza fursa mbalimbali zinazotolewa na CPB kwa wakulima na wafanyabiashara wa Mazao hapa nchini, ikiwemo kilimo cha mkataba ambacho kitaanzia na ekari 1000 na kuendelea.

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika mjini Iringa, Awadh alisema Kilimo cha mkataba cha CPB kitakuwa cha uhakika kwa wakulima ambao watapata mazao yaliyo katika ubora sambamba na fursha nyingine kuhitajika kwa Mawakala watakaoingia nao mkataba kwaajili ya uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa na CPB na kununua mazao ya wakulima na Wafanyabishara.

Amesema, “CPB ni Shirika la Kibiashara la Serikali hivyo linafanya biashara kwa lengo la kuinua Uchumi wa nchi lakini na mtu mmoja mmoja, bashara ambayo CPB inafanya hatuwezi kumlalia mkulima au mfanyabiashara wa mazao, sisi lengo letu tupate na wao wapate.”

Aidha, Awadh alisema CPB inaongezea thamani mazao kwa kuchakata mazao kama Mpunga, Mahindi, Ngano, Alizeti na Siagi kupitia Viwanda vya CPB vilivyopo katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Iringa na kuwataka wafanyabiashara na wakulima wa mazao watumie fursa hiyo, ili kuinua uchumi wao.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa  Iringa, Elia Luvanda aliitaka CPB kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha unga wa lishe kwa ajili ya Wanafunzi mashuleni.

“Unajua ukanda huu wa Nyanda za juu kuna tatizo la watoto kukosa lishe,hivyo niwaombe CPB mbali na kufanya biashara ya mazao,wajenge kiwanda cha kutengeneza lishe ili watoto wetu waondokane na utapiamlo,” alisema Luvanda.

Odds Kubwa za Ushindi ni Hizi
Victor Osimhen pasua kichwa Ulaya