Ukatili wa kijinsia na unyanyasaji mahala pakazi umetajwa kuzidi kushamiri ambapo katika maeneo mengi ya kazi, wafanyakazi wengi hasa wanawake wamekuwa hawapewi fursa ya kuonesha uwezo wao.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania – TUCTA, Rehema Ludanga wakati izungumza na waandishi wa habari mkoni Morogoro.
Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania – TUCTA, Rehema Ludanga.
Amesema, katika kuadhimisha ya siku ya wafanyakazi Duniani ni vyema serikali ikaandalia kwa kwa umakini maswala ya ukatili wa kijinsia, kwani changamoto hiyo ni kubwa na huwakuta hadi viongozi walio kwenye ngazi mbalimbali za kiutendaji.
“Nitumie fursa hii wakati tukiadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani kuwaomba viongozi hasa wanaume waache unyanyasaji wa kijinsia, kama kuna kiongozi mwanamke apewe fursa kulingana nafasi yake, kama kunamfanya kazi mwanamke apewe nafasi yake bila ya kujali jinsi,” alisema Ludanga.