Waumini wa Kanisa Assemblies of God – TAG, wamefanya ibada ya kuliombe Taifa na Viongozi wake, katika kilele cha Siku ya Wanaume Wakristo, huku Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa akishiriki ibada hiyo na kuwasihi kuliombea Taifa baraka, utulivu na amani.

Ibada hiyo, imefanyika Mkoani Mbeya na imeongozwa na Mchungaji wa Kanisa hilo, Amnon Mwakitalu ambapo pia Mkuu huyo wa Wilaya aliwasisitiza waumini suala la umoja na mshikamano.

Alisema, ili Taifa liweze kuongozwa vyema ni jukumu la kila mmoja kuwaombea Viongozi wa Taifa wakiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, wasaidizi wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt Tulia Ackson.

Mkuu huyo wa Wilaya, kwa nyakati tofauti amekuwa akisisitiza suala la kuzingatia maadili kwa watumishi wa wa Serikali, usafi miongoni mwa jamii na kuhakikisha huduma za kijamii zinatolewa kwa weledi na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu.

Mkutano wa dharula wamfikisha Rais Samia Namibia
George Mpole asaka njia ya kujinasua DR Congo