Kesi iliyowasilishwa Mahakamani na Muhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New Life International Ministries dhidi ya serikali, itaendelea tena kesho Jumanne Mei 9, 2023.

Hatua hiyo inatokana na uamuzi uliotolewa na Jaji Mahakama Kuu ya Mombasa, Olga Sewe baada ya upande wa mashtaka kuomba muda zaidi wa kuwasilisha majibu.

Muhubiri Ezekiel ameishtaki serikali kwa kufunga kituo chake cha runinga na kanisa lake akidai uamuzi huo haukufanywa kisheria bali yalikuwa maamuzi ya watu binafsi.

Serikali kufanya maboresho Elimu ya awali, msingi
Pialali kukiwasha Dar es salaam Mei 27