Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu kuokolewa baada ya mtumbwi waliokuwa wakifanyia shughuli za uvuvi kuzama katika Ziwa Victoria Mkoani Geita.

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Geita, Wambura Fidel amesema wakati wavuvi hao wakitekeleza majukumu katika mtumbwi walikuwa sita, na watatu kati yao Kurwa Thomasi (30), Dicksoni Alphonce ( 47), na Dickson Majura ( 22) waliokolewa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Corlnery Magembe amewapa pole wafiwa na kuwasihi wale wote wanaojihusiha na uvuvi wilayani humo kuhakikisha wanazingatia taratibu za usalama majini na kuchukua tahadhari wakati na kabla ya majanga.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 10, 2023
Kondoa wahimizwa miradi ya uhimili mabadiliko tabianchi