Mkuu wa Benchi la Ufundi la Azam FC Kally Ongala ametengeneza Rekodi ya kibabe akiwa na timu hiyo tangu alipochukua mikoba ya aliyekuwa kocha wao mkuu Denis Lavagne, huku akisema anataka ubingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ unaoshikiliwa na Young Africans.

Kally alirithi mikoba ya Lavagne ambaye alitupiwa virago baada ya timu hiyo kuwa na matokea yasiyofurahisha.

Kocha huyo ametengeneza Rekodi ya kutofungwa na Simba SC kwenye Ligi Kuu hadi Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, ambapo kwenye ligi mchezo wa kwanza Azam FC ilishinda bao 1-0, kisha mchezo wa pili timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Pia amehakikisha timu hiyo hadi sasa ipo nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ikiwa na alama 53 katika mechi 27 ambazo imecheza hadi sasa na hali hiyo imejihakikishia kucheza mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao.

Katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ uliochezwa Jumapili (Mei 07), kocha huyo akiwa kwenye benchi la Azam FC alitengeneza rekodi nyingine na kwa timu yake kwa kuifunga Simba SC mabao 2-1 na kutinga Fainali ya mashindano hayo ikisubiri kwa sasa mshindi kati ya Singida Big Stars dhidi ya Young Africans.

“Malengo yetu yalikuwa ni kuchukua ubingwa wowote kwa hiyo kwa sasa akili yetu ipo huku tulipoingia fainali, tukichukua ubingwa ndio jambo kubwa kwetu kwa sababu tutakuwa tumetimiza lengo.” amesema

Azam FC itatakiwa kuichapa Young Africans au Singida Big Stars kwenye mchezo wa Fainali ili iweze kutwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu huu 2022/23.

Mwingine aokolewa shambani kwa mchungaji Mackenzie
Halmashauri yatakiwa kukamilisha mradi ndani ya Julai