Maafisa wa upelelezi wamemkamata mwanaume mmoja na kuokoa mwengine ambao idadi yao haijatajwa katika oparesheni ya msako inayoendelea katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi lililopo Malindi Pwani ya Kenya.

Huku hayo yakijiri shughuli ya kutoa chembechembe za vinasaba kutoka Kwa familia zilizopoteza jamaa zao inaendelea katika hospitali Malindi, ikitarajiwa kuchukua mwezi mzima kulinganisha vinasaba vya wafu na familia.

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya, Kithure Kindiki hivi karibuni alisema Serikali itaweka kila kitu wazi baada ya uchunguzi huo ikiwemo miili ambayo itapatikana bila baadhi ya viuongo akidai kuwa serikali haifichi chochote.

Uchunguzi wa miili hiyo unaendeshwa na  kikosi cha watalamu kinchongozwa na mwanapathologia mkuu wa Serikali, Dkt. Johansen Oduor katika makafani ya Hospitali ya Malindi.

Babi aipeleka Young Africans fainali
Simba SC yamwandikia rekodi Kocha Azam FC